IQNA – Hafla ya kufunga awamu ya mwisho ya Mashindano ya 48 ya Kitaifa ya Qur'an ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inatarajiwa kufanyika, Oktoba 27, katika mji wa Sanandaj, mkoa wa Kordestan.
Habari ID: 3481420 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/26
IQNA – Washiriki wa kitengo cha wanawake katika Mashindano ya 48 ya Kitaifa ya Qur’ani Tukufu nchini Iran waliendelea kuonesha umahiri wao siku ya tatu ya mashindano hayo, wakishindania nafasi za juu.
Habari ID: 3481412 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/25
IQNA – Kongamano la kwanza la kimataifa la “Qur’an ya Negel” limefanyika mjini Sanandaj siku ya Jumatatu, likiwakutanisha makari na wahifadhi wa Qur’an wanaozungumza Kikurdi kutoka Iran, Uturuki na Iraq.
Habari ID: 3481394 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/21
IQNA-Sheikh Mamosta Fayeq Rostami, msomi maarufu wa Ahul Sunna na mwakilishi wa watu wa Kurdistan katika Baraza la wanazuoni Wataalamu wanaomchagua Kiongozi Muadhamu wa Iran amesisitiza kuwa Qurani Tukufu si tu kitabu cha ibada, bali ni waraka kamili unaoelekeza maisha ya binadamu katika nyanja za uchumi, utamaduni na siasa
Habari ID: 3481387 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/20
IQNA-Awamu ya mwisho ya Mashindano ya Kitaifa ya Qur’ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya 48 imezinduliwa rasmi katika hafla iliyofanyika asubuhi ya Jumamosi katika mji wa Sanandaj, mkoa wa Kurdistan.
Habari ID: 3481386 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/19
IQNA – Mashindano ya 48 ya Kitaifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran, yakihusisha washiriki 330 kutoka maeneo mbalimbali ya nchi, yatafanyika mwaka huu katika mji wa Sanandaj ulioko magharibi mwa Iran, chini ya kauli mbiu: “Qur'ani, Kitabu cha Umoja.”
Habari ID: 3481362 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/13
IQNA – Siku ya kwanza ya mashindano ya kitaifa ya Qur’ani yajulikanayo kama “Zayin al-Aswat” (mapambo ya sauti) ilianza rasmi Jumatano mjini Qom, yakikusanya vijana wasomaji wa Qur’ani kutoka pembe zote za Iran.
Habari ID: 3481317 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/02
IQNA – Mkurugenzi mtendaji wa toleo la kwanza la mashindano ya Qur'ani ya kitaifa ya ‘Zayin al-Aswat’ (mapambo ya sauti) amesema kuwa katika mashindano mengi ya Qur'an, kila kitu huisha kwa sherehe ya kufunga na kuwatuza washindi na sasa sekretarieti ya tukio hili la Qur'an inalenga kuandamana na washiriki kupitia mawasiliano endelevu na yenye tija ili kuwafikisha katika viwango vya kitaalamu na vya kimataifa.
Habari ID: 3481314 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/01
IQNA – Mkutano maalum umefanyika mjini Tehran kujadili ‘Mpango wa Kiutendaji na Ramani ya Njia ya Kuwafundisha Waislamu Milioni 10 Kuhifadhi Qur’ani’.
Habari ID: 3481308 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/30
IQNA – Taasisi ya Mahd Qur'ani ya Iran imetoa vyeti 1,004 kwa wanafunzi waliokamilisha kuhifadhi sura za Qur'ani Tukufu na kuelewa maana ya aya zake katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo ya mwaka wa sasa wa kalenda ya Ki iran i (ulioanza Machi 21).
Habari ID: 3481301 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/29
IQNA – Ahmad Abolqassemi, Qari mashuhuri kutoka Iran, amesisitiza uwezo wa kipekee wa nchi hiyo katika uwanja wa usomaji wa Qur’ani Tukufu, akipendekeza kuandaliwa mashindano mapya ya kipekee ya “fainali ya mabingwa” kwa washindi wa mashindano ya kimataifa ya Qur’ani, yatakayofanyika nchini Iran.
Habari ID: 3481300 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/29
IQNA – Toleo la kwanza la mashindano ya kitaifa ya Qur’ani ya Iran ya “Zayin al-Aswat” (mapambo ya sauti) linatarajiwa kufanyika katika mji mtakatifu wa Qom, likijumuisha makundi matatu kuu, waandaaji walitangaza.
Habari ID: 3481298 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/28
IQNA-Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Tafsiri ya Qur’ani na Maandishi ya Kidini nchini Iran, Karim Dolati, ametangaza kuwa taasisi hiyo imekagua kati ya tafsiri 40 hadi 50 za Qur’ani Tukufu na kazi zinazohusiana katika kipindi cha miezi sita iliyopita.
Habari ID: 3481292 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/27
IQNA – Idadi ya safari za ndege zinazowasafirisha waumini wa ibada ya Umrah kutoka Iran kwenda Saudi Arabia imeongezeka tangu mwanzo wa wiki hii.
Habari ID: 3481287 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/26
IQNA-Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani mashambulizi ya anga ya “kikatili” yaliyofanywa na Marekani na Israel mwezi Juni katika ardhi ya Iran na kusema yalikuwa usaliti kwa diplomasia.
Habari ID: 3481282 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/25
IQNA – Majina ya wale wanaostahiki kushiriki katika hatua ya fainali ya Mashindano ya 48 ya Kitaifa ya Qur’ani Tukufu nchini Iran yametangazwa.
Habari ID: 3481277 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/24
IQNA – Mwanazuoni na mwanaharakati kutoka Malaysia ametoa wito kwa Waislamu kote duniani kuonesha mshikamano kwa vitendo badala ya maneno, akisisitiza kuwa Qibla ya pamoja inapaswa kuwa msingi wa mshikamano wa Ummah.
Habari ID: 3481275 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/23
IQNA – Waziri wa Mambo ya Kidini wa Pakistan ametoa mwaliko rasmi kwa wataalamu na wasomaji wa Qur’ani kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kushiriki katika Mashindano ya Kwanza ya Kimataifa ya Usomaji wa Qur’ani yanayotarajiwa kufanyika nchini humo.
Habari ID: 3481274 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/23
IQNA – Mwanasiasa na mchambuzi wa masuala ya kisiasa kutoka Iran ametoa wito kwa nchi zenye Waislamu wengi kuunda umoja wa kisiasa na kiuchumi ili kuimarisha msimamo wao wa pamoja dhidi ya miungano ya mataifa ya Magharibi kama vile NATO na Umoja wa Ulaya.
Habari ID: 3481270 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/22
IQNA – Kwa mwaname mmoja kutoka Iran ambaye ameweka juhudi kwa muda wa miongo miwili kuhifadhi Qur’ani Tukufu, kitabu hiki kitakatifu si tu maandiko ya kidini, bali ni mwongozo wa kibinafsi na chemchemi ya utulivu wa kina.
Habari ID: 3481269 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/22