IQNA

Jumba la Makumbusho la Mazulia ya Iran katika Picha

IQNA - Jumba la Makumbusho la Mazulia la Iran, lenye eneo la mita za mraba 3,400, linaonyesha mkusanyiko wa takriban mazulia 2,000 za Kiajemi tokea enzi ya Safavid hadi sasa.

Mkusanyiko huo unajumuisha aina mbalimbali mazulia. Jumba la makumbusho lililoko kaskazini-magharibi mwa Bustani ya Laleh jijini Tehran, liliongezwa kwenye Orodha ya Turathi ya Kitaifa mnamo Novemba 2017.

Picha zifuatazo zimepigwa tarehe 9 Juni 2024, ambayo inaadhimisha siku ya kitaifa ya mazulia nchini Iran.