Na humo watanyweshwa kinywaji kilicho changanyika na tangawizi.
Na humo watanyweshwa kinywaji kilicho changanyika na tangawizi.
Na watawazungukia kuwatumikia wavulana wasio pevuka, ukiwaona utawafikiri ni lulu zilizo tawanywa.
Na utakapo yaona, utakuwa umeona neema na ufalme mkubwa.
Juu yao zipo nguo za hariri laini za kijani kibichi, na hariri nzito ya at´ilasi. Na watavikwa vikuku vya fedha, na Mola wao Mlezi atawanywesha kinywaji safi kabisa.
Hakika haya ni malipo yenu; na juhudi zenu zimekubaliwa.
Hakika Sisi tumekuteremshia Qur´ani kidogo kidogo.