Barre alitoa kauli hiyo wakati wa hafla rasmi ya uzinduzi wa mashindano ya kila mwaka ya usomaji wa Qur'ani yaliyofanyika katika mji mkuu, Mogadishu.
Tukio hilo lina lengo la kuendeleza elimu ya dini na kuimarisha mshikamano miongoni mwa jamii ya Wasomali. Waziri Mkuu alisisitiza jukumu muhimu la wanazuoni wa Somalia katika kuwaelekeza vijana kupitia mafundisho ya Qur'ani, maadili ya Kiislamu, na Sunnah.
Aliangazia umuhimu wa kulea kizazi chenye misingi imara ya elimu ya dini na maadili, akibainisha kuwa hii itasaidia kupambana na itikadi kali na kuzuia upotoshaji wa Uislamu, ambao umesababisha umwagaji damu kwa watu wa Somalia.
"Mashindano ya Qur'ani ni jukwaa la kuleta umoja ndani ya jamii yetu, likikuza mshikamano na mshikano kati ya Waislamu. Tunakumbushwa umuhimu wa kushikamana na mafundisho ya Qur'ani na Sunnah katika maisha yetu ya kila siku, kwani hutuelekeza katika kulinda imani yetu na kutii amri za Mwenyezi Mungu," alisema Barre.
Aidha, aliwataka wanazuoni wa Somalia kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya makundi yenye itikadi kali na kupinga fikra potofu zinazopotosha maana halisi ya Uislamu.
Somalia inmekuwa ikishuhudia mashambulizi ya makundi ya kigaidi, hasa kundi la kigaidi la Al Shabab, ambalo limepelekea maelfu ya watu kuuawa nchini humo na maelfu kuachwa bila makao.
3492283