IQNA

Kwa mujibu wa riwaya kutoka kwa Maimamu Watoharifu AS, moja ya maeneo yenye thamani kubwa zaidi ardhini ni ardhi ya Karbala. Eneo hilo ni jiografia nyekundu ya maashiki wa Imam Hussein AS ambao kwa kupokea mwaliko kutoka kwa Bwana wa Mashahidi, zikiwa zimesalia siku chache kabla ya Ashura ya Imam Hussein AS, wamesafiri katika ardhi hii takatifu ili nyoyo ziwe hapo katika wakati muafaka.