IQNA

TEHRAN (IQNA) – Sherehe inayojulikana kama Ajvatovica imefanyika nchini Bosnia na Herzegovina kuadhimsiha mwaka 510 tokea Uislamu uingie nchini humo.

Ajvatovica ni sherehe kubwa zaidi ya Kiislamu barani Ulaya na imefanyika wiki iliyopita karibu na eneo la Prusac, nchini Bosnia na Herzegovina. Sherehe hiyo imepewa jina la Ajvaz-dedo, mzee mcha Mungu aliyeikuwa na mchango mkubwa katika kueneza Uislamu eneo hilo.

Sherehe hiyo ya siku saba ilihudhuriwa na idadi kubwa ya Waislamu ambao hushiriki pamoja katika swala za jamaa.