IQNA

Washiriki 160 wafuzu kwa fainali za Mashindano ya Kimataifa ya Qur'an katika Ukanda wa Balkan

15:14 - April 20, 2025
Habari ID: 3480569
IQNA – Mchujo wa awali wa mashindano makubwa zaidi ya kimataifa ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu katika ukanda wa Balkan umekamilika huko Bosnia na Herzegovina.

Wizara ya Mambo ya Kiislamu, Daawa na Mwongozo ya Saudi Arabia, kupitia Mwambata wa Kidini katika ubalozi wa nchi hiyo ya Kiarabu nchini Bosnia na Herzegovina, ndio iliendesha raundi ya awali.

Hii ni mara ya tatu kwa tukio hili kufanyika, likiwa limeandaliwa kwa ushirikiano na Sheikhe Mkuu wa Kiislamu wa Jamhuri ya Kosovo na kwa uratibu na Ubalozi wa Saudi Arabia katika Jamhuri ya Albania.

Mashindano haya yalishirikisha washiriki 2,350 kutoka nchi 22, zikiwemo Kosovo, Albania, Bosnia na Herzegovina, Montenegro, Macedonia ya Kaskazini, Italia, Uturuki, Ugiriki, Bulgaria, Jamhuri ya Czech, Cyprus, Slovenia, Croatia, Romania, Serbia, Estonia, Ubelgiji, Ukraine, Georgia, Urusi, Belarus, na San Marino.

Jumla ya washiriki 160 wamefuzu kwa raundi ya fainali, ambayo itafanyika kuanzia Mei 8 hadi 11 katika mji mkuu wa Kosovo, Pristina, ambako watachuana katika makundi matano tofauti.

Jumla ya zawadi katika mashindano haya ni SAR 500,000, huku gharama ya maandalizi ya tukio hilo ikikadiriwa kufikia SAR 1.2 milioni.

3492750

captcha