IQNA – Kitendo cha kudhalilisha na kuivunjia heshima Qur’ani Tukufu kilichotokea mjini Plano, jimbo la Texas, Marekani, kimezua hasira kubwa miongoni mwa wananchi na mashirika ya haki za binadamu.
Habari ID: 3481659 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/12/14
IQNA – Katika jiji la Dearborn, Michigan, kuna taasisi ya Kishia iliyodumu kwa miaka mingi, ikifanya kazi kimya kimya bila makuu, lakini ikiwa na athari kubwa katika jamii.
Habari ID: 3481658 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/12/14
IQNA – Kituo cha Kimataifa cha Uislamu kwa Uvumilivu na Amani nchini Brazil kimeanzisha mpango maalumu wa kielimu wiki hii katika uwanja wa tafsiri ya Qur’ani Tukufu na kusoma Hadith za Mtume (SAW).
Habari ID: 3481618 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/12/05
IQNA – Seneta mwenye msimamo mkali wa mrengo wa kulia nchini Australia, Pauline Hanson, ameibua hasira kali Jumatatu baada ya kuingia bungeni akiwa amevaa vazi la Waislamu la burka, kama sehemu ya juhudi zake za mara kwa mara za kutaka vazi hilo lipigwe marufuku kwa sababu eti wanaovaa hufunika uso wote hadharani.
Habari ID: 3481565 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/25
IQNA – Mashirika kadhaa ya Kiislamu nchini Ufaransa yamekosoa taasisi ya utafiti wa maoni ya wananchi, IFOP, kwa kile walichokiita upendeleo wa wazi na kuvunja viwango vya maadili ya kitaaluma.
Habari ID: 3481564 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/25
IQNA – Mkutano wa 38 wa Kimataifa wa Waislamu wa Amerika ya Kusini na Karibiani unafanyika nchini Brazil, ukikusanya viongozi wa Kiislamu kujadili mada ya vijana Waislamu katika enzi ya akili mnemba (AI).
Habari ID: 3481553 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/22
IQNA – Kamati ya Masuala ya Katiba ya Ureno imeamua kuwa pendekezo la kuzuia ufadhili wa umma kwa ujenzi wa misikiti halina msingi wa kikatiba.
Habari ID: 3481549 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/21
IQNA – Baada ya tukio la uhalifu wa chuki lililoripotiwa ambapo dada Muislamu alivamiwa na kufuatwa karibu na Chuo Kikuu cha Columbia kwa sababu ya kuvaa niqab, taasisi hiyo imetoa tamko la kulaani shambulio hilo hadharani.
Habari ID: 3481522 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/16
IQNA – Mradi wa kutafsiri Qur'an kwa lugha ya Rohingya umeanzishwa katika mazingira ambapo Waislamu wa Rohingya wamekuwa wakilengwa na dhulma na kufukuzwa kutoka ardhi yao kwa miongo kadhaa. Lengo lake ni kuziba pengo la maarifa ya Kiislamu na kupambana na ukandamizaji wa lugha ya Rohingya.
Habari ID: 3481493 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/09
IQNA-Katika ripoti mpya iliyotolewa na taasisi ya utafiti ya Uswidi, imebainika kuwa idadi kubwa ya wanafunzi Waislamu wamekuwa wakihama shule kutokana na kukumbwa na ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya Uislamu.
Habari ID: 3481482 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/07
IQNA-Zohran Mamdani mbunge Muislamu amechaguliwa kuwa Meya wa 111 wa jiji la New York, mtu wa kwanza mwenye asili ya Asia Kusini na wa kwanza aliyezaliwa barani Afrika kuongoza jiji kubwa zaidi nchini Marekani.
Habari ID: 3481471 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/05
IQNA – Imamu Mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar nchini Misri, Sheikh Ahmad al-Tayyib, amesema kuwa dunia inakumbwa na machafuko na ukosefu wa mantiki, hali ambayo chanzo chake ni kupuuzwa kwa maadili ya kidini na kiutu.
Habari ID: 3481456 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/03
IQNA – Kupitia ukurasa wake wa Facebook, mhadhiri wa chuo kikuu kutoka Misri, Sayed Sharara, amefungua dirisha la kipekee kuonesha maisha ya Waislamu nchini Japani.
Habari ID: 3481455 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/03
IQNA – Polisi nchini New Zealand wanafanya uchunguzi kuhusu tishio la bomu lililolenga Msikiti wa Kilbirnie uliopo Wellington, hali iliyosababisha kusitishwa kwa shughuli zote za msikiti huo kwa muda.
Habari ID: 3481411 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/25
IQNA – Mtandao wa Mazungumzo ya Kiislamu nchini Norway (Islamic Dialogue Network) umezindua tovuti ya kwanza ya kitaifa ya kupambana na chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia), iitwayo stoppmuslimhat.no.
Habari ID: 3481403 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/23
IQNA- Kufuatia ongezeko kubwa la uhalifu wa chuki dhidi ya Waislamu nchini Uingereza, serikali inatarajiwa kutangaza ufafanuzi mpya wa neno “'Chuki Dhidi ya Uislamu' (Islamophobia)”—ambapo huenda likabadilishwa na kuwa “chuki dhidi ya Waislamu.”
Habari ID: 3481402 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/23
IQNA – Jumuiya ya Waislamu wa jiji la Winnipeg, mji mkuu wa jimbo la Manitoba nchini Kanada (Canada), walikusanyika mwishoni mwa wiki hii kusherehekea ufunguzi rasmi wa msikiti mpya katika jiji hilo.
Habari ID: 3481392 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/21
IQNA – Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Itikadi Kali kimetoa onyo kali kuhusu matumizi mabaya ya teknolojia ya Akili Mnemba (AI) katika kuchochea chuki dhidi ya Waislamu nchini India.
Habari ID: 3481391 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/21
IQNA – "Misikiti katika Uislamu" ni jina la maonyesho ya sanaa yaliyozinduliwa katika Msikiti Mkuu wa Paris, mji mkuu wa Ufaransa.
Habari ID: 3481379 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/18
IQNA – Maktaba ya Kitume ya Vatican imetenga eneo dogo kwa ajili ya watafiti Waislamu kuswali wanapoitembelea.
Habari ID: 3481369 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/15