IQNA

Ayatullah Mohammad Ali Taskhiri; sauti yenye mvuto ya Uislamu na Ushia

TEHRAN (IQNA) - Ayatullah Ali Taskhiri, mshauri mwandamizi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu masuala ya ulimwengu wa Kiislamu alikuwa mmoja kati ya walinganiaji wa umoja na ukuruba baina ya madhehebu za Kiislamu.

Ayatullah Taskhiri, aliaga dunia na kurejea kwa Mola wake Jumanne Agosti 18 2020 mjini Tehran akiwa na umri wa miaka 76. Mwanazuoni huo mtajika aliaga dunia hospitalini kutokana na matatizo ya moyo.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei alituma salamu za rambirambi kwa mnasaba wa kuaga dunia mwanazuoni, mujahid na mtetezi wa Uislamuna kumtaja kuwa sauti yenye mvuto ya Uislamu na Ushia.