IQNA

TEHRAN (IQNA)- Vijana Wapalestina wapatao 140 ambao wamehifadhi Qur’ani Tukufu wameshiriki katika matembezi huko katika Ukanda wa Ghaza.

Matembezi hayo yameandaliwa na Msikiti wa Al Abrar chini ya kauli mbiu ya ‘nyuso zilizonawiri’.

Katika hafla hiyo vijana 140 waliohifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu walishiriki katika matembezo hayo katika mitaa ya Rafah huku wakiwa wamevalia mavazi meupe.

Kauli mbiu ya matembezi hayo imetokana na aya ya 38 ya Sura Abasa katika Qur’ani Tukufu isemayo:

 “Siku hiyo ziko nyuso zitazo nawiri”

Msikiti wa Al Abrar uko mstari wa mbele katika kuwafunza watoto masomo mbali mbali ya Qur’ani Tukufu.

Quran Memorizers March in Gaza

Quran Memorizers March in Gaza

3999755