IQNA

Msomaji Qur'ani

Qari Mahmoud Shahat Anwar wa Misri Asoma Qur'ani nchini Comoro (+Video)

TEHRAN (IQNA) – Qari mashuhuri wa Misri Mahmoud Shahat Anwar amesafiri kwenda Visiwa vya Comoro kusoma Qur'ani Tukufu huko katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Anwar Shahat Anwar ni mwanae marhum Sheikh Muhammad Shahat Anwar na alizwaliwa mwaka 1979.

Alifanikiwa kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu akiwa na umri wa miaka 12 kutoka kwa baba yake. Ameweza kuibuka mshindi katika mashindano mengi ya Qur'ani ya kitaifa na kimataifa. Sheikh Mahmod Shahat Muhammad Anwar  amewahi kusafiri katika nchi nyingi duniani kushiriki katika mashindano ya Qur'ani ikiwa ni pamoja na Iraq, Iran, Qatar, UAE, Algeria, Syria, Pakistan, Afrika Kusini, Ugiriki, Uturuki na Ubelgiji.

Comoro ni visiwa vya volkeno karibu na pwani ya mashariki ya Afrika, katika maji ya joto ya Bahari ya Hindi katika eneo la Mfereji wa Msumbiji. 
Uislamu ndiyo dini kubwa zaidi nchini Comoro ambapo takriban asilimia 98 ya wakazi wanakadiriwa kufuata dini hiyo.
Ufuatao ni usomaji wa Mahmoud Shahat Anwar wa aya kutoka za Surah Ash-Shams katika mahafali ya Qur'ani huko Comoro.
4134705
Kishikizo: sahat anwar