IQNA

Harakati za Qur'ani Misri

Wasomaji Qur'ani maarufu wahudhuria uzinduzi wa msikiti huko Qalyubia nchini Misri

20:48 - November 26, 2022
Habari ID: 3476151
TEHRAN (IQNA) - Baadhi ya maqarii au wasomaji maarufu zaidi wa Qur'ani Tukufu walihudhuria sherehe za uzinduzi wa msikiti katika Jimbo la Qalyubia nchini Misri.

Hafla hiyo ilifanyika Ijumaa jioni kuzindua Msikiti wa Bahri huko Tant Al-Jazira katika mkoa wa kaskazini, tovuti ya habari ya al-Bawaba iliripoti.

Qalyubia iko kaskazini mwa Cairo katika eneo la Delta ya Nile na mji mkuu wake ni Banha.

Mahmoud Shahat Anwar, Yassir al-Sharqawi, Shahat al-Sayyed A’azazi na Sheikh Mohamed Abdul Qadir walikuwa miongoni mwa wasomaji mashuhuri waliokuwepo kwenye hafla hiyo.

Kulikuwa pia na wanaharakjati wengine wa Qur'ani, wanazuoni na wasomi wa Qur'an na shakhsia wengine kidini katika televisheni waliohudhuria sherehe hiyo.

Maqarii walisoma aya za Qur'ani Tukufu na Sheikh Mohamed Abdul Qadir aliwasilisha Ibtihal  katika sherehe ya uzinduzi.

Misri ni nchi ya Afrika Kaskazini yenye wakazi wapatao milioni 100.

Waislamu ni takriban asilimia 90 ya watu wote wa nchi hiyo.

Shughuli za Qur'ani ni maarufu  sana katika nchi hii ambayo ina idadi kubwa zaidi ya wasomaji bingwa wa Qur'ani Tukufu duniani.

Top Qaris Attend Inauguration of Mosque in Egypt’s Qalyubia  

Top Qaris Attend Inauguration of Mosque in Egypt’s Qalyubia  

Top Qaris Attend Inauguration of Mosque in Egypt’s Qalyubia  

 

4102353

Kishikizo: misri ، qurani tukufu ، waislamu
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha