Tukio hilo lilihudhuriwa na mfawidhi wa Idara ya Haram ya Imam Ridha (AS) ambayo inajulikana kama Astan Quds Razavi , pamoja na kundi la wanazuoni, familia za mashujaa waliouawa shahidi, wasanii, watumishi wa haram, na wananchi wa kawaida.
Wiki ya Karamat huadhimisha siku za kuzaliwa kwa Hazrat Masoumah (SA) na Imam Ridha (AS), ambazo mwaka huu zinaangukia tarehe 29 Aprili na 9 Mei, mtawalia. Ni kipindi cha Ziyara katika maeneo hayo mawili matakatifu, sherehe, na matukio ya kitamaduni, hasa katika miji kama Mashhad na Qom.
Chanzo za picha:razavi.ir