Kumbukumbu ya shahada ya Imam Ridha (AS) mwaka huu itasadifiana na Jumapili, tarehe 24 Agosti 2025 ambayo itakuwa ni siku kuu ya kitaifa nchini Iran. Siku hii huangukia tarehe 30 ya mwezi wa Safar katika kalenda ya Kiislamu.
Katika miaka ya karibuni, mamilioni ya waumini wamekuwa wakishiriki katika ziyara hii. Mnamo mwaka 2024, zaidi ya watu milioni tano walikusanyika mjini Mashhad katika hafla za maombolezo
Desturi hii hujumuisha misafara ya kutembea kutoka miji na mikoa iliyo karibu, huku mamia ya maelfu wakikamilisha safari yao kwa miguu.
Imam Ridha, ambaye ni Imam wa nane katika madhehebu ya Shia Ithna Ashariyya, aliuawa kwa sumu mnamo mwaka 203 Hijria Qamariya (818 Miladia) na Khalifa wa Abbasiyya, Al-Ma’mun. Kaburi lake takatifu liko mjini Mashhad, na hapo ndipo kulipojengwa Haram Tukufu. Kwa karne nyingi eneo hilo limekuwa miongoni mwa vituo vinavyotembelewa sana duniani na wafanyaziyara.
4300988