IQNA

Zaidi ya Watoto 3,000 washiriki hafla ya Qur’ani Katika Haram ya Imam Ridha (AS) + Picha

16:49 - August 20, 2025
Habari ID: 3481111
IQNA – Zaidi ya watoto 3,000 wamekusanyika katika Haram Tukufu ya Imam Ridha (AS) mjini Mashhad kwa ajili ya kongamano la Qur’ani lililopewa jina “Malaika wa Muqawama (Upinzani)”, na kujaza eneo hilo tukufu kwa tilawa na sauti za imani.

Hafla hiyo, iliyofanyika katika ukumbi wa Imam Khomeini wa Haram siku ya Jumanne, iliandaliwa na Kituo cha Masuala ya Qur’ani cha Astan Quds Razavi.

Mkusanyiko huu, uliotimia katika siku za mwisho za mwezi wa Safar, ulikuwa na lengo la kuimarisha uhusiano wa watoto na Qur’an Tukufu. Miongoni mwa shughuli, kulikuwa na hati kubwa ya maandiko ya kulaani jinai za Kizayuni dhidi ya Wapalestina na mataifa mengine, iliyosainiwa na watoto hao. Waandalizi walisema hati hiyo itapelekwa UNESCO kwa lugha mbalimbali kama “sauti ya watoto waliodhulumiwa duniani kote.”

Mwito wa haki ulijiri pia baada ya uvamizi wa karibuni wa utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran. Mnamo Juni 13, utawala huo ulianzisha vita kamili vya kijeshi ndani ya ardhi ya Iran, ukishambulia maeneo ya kijeshi na nyuklia, na kuwaua makamanda wa ngazi ya juu, wanasayansi na raia wasio na hatia, wakiwemo watoto.

Marekani pia ilijiunga na vita hivyo kwa kulenga vituo vya nyuklia vya Iran. Kwa kujibu, Iran ilipiga kwa makombora sahihi vituo vya kijeshi vya Kizayuni na kuushambulia kambi ya kijeshi ya Marekani nchini Qatar. Baada ya siku 12 za mashambulizi na mashambulizi ya kulipiza kisasi, utawala wa Kizayuni ulilazimishwa kutangaza kusitisha mapigano kwa upande mmoja.

“Hati hii inaakisi uamsho na kilio cha watoto wasio na hatia duniani kote,” alisema Hujjat al-Islam Masoud Mirian, Mkuu wa Kituo cha Qur’ani cha Haram Tukufu, katika maelezo yake pembeni ya hafla hiyo.

Viongozi wa kikao waligusia pia kujitolea binafsi. Bi. Zahra Mesbah, mjane wa shahidi Ahad Aqdasi na mama wa watoto wawili mashahidi, Mohaddeseh (13) na Mohammadreza (9), alieleza uimara wa imani ya watoto wake. Alisema kuwa mapambano kati ya haki na batili yapo “tangu mwanzo wa uumbaji” na akasisitiza wajibu wa kubaki na matumaini na subira.

Mama wa shahidi Danial Rezazadeh, afisa wa usalama, naye alitoa ushuhuda akisema mwanawe pekee “alijitolea uhai wake kwa ajili ya usalama na heshima ya taifa” na alifariki dunia wakati wa Swala ya Magharibi.

3494326

Habari zinazohusiana
captcha