Msikiti wa Kifalme (Badshahi), Lahore, Pakistan
Msikiti wa Kifalme (Badshahi Masjid) uko mjini Lahore, katika jimbo la Punjab nchini Pakistan. Jina rasmi la msikiti huo ni Masjid Abul Zafar Muhy-ud-Din Mohammad Alamgir Badshah Ghazi na ulijengwa wakati wa silsila ya ufalme wa Aurangzeb kati ya mwaka 1671 na 1673 Miladia. Msikiti huo ni nembo muhimu ya usanifu majengo wa Kiislamu nchini Pakistan na ni msikiti wa pili kwa ukubwa nchini humo na wa tano kwa ukubwa duniani.