iqna

IQNA

iqna
Harakati za Qur'ani
IQNA - Taasisi moja ya Kiislamu nchini  Iran imetangaza kuwa imekamilisha tafsiri ya Kiswidi ya Qur'ani Tukufu katika hatua ya "kupambana na ujahilia" au ujingakufuatia matukio kadhaa ya kuvunjiwa heshima Qur'ani nchini humo mwaka jana.
Habari ID: 3478639    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/06

Maadhimisho
IQNA- Makumi ya maafisa na wanaharakati wa Qur'ani wameadhimisha mwaka wa 21 wa kuanzishwa kwa kwa Shirika la Kimataifa la Habari za Qur'ani (IQNA).
Habari ID: 3478593    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/28

Watetezi wa Qur'ani Tukufu
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Duniani (IUMS) aliona kususia huko kuwa chombo madhubuti dhidi ya nchi zinazounga mkono kuchomwa moto kwa Qur'ani Tukufu na akasema: Kususia ni mapinduzi na matakwa ya halali. Akizungumza katika kongamano la watetezi wa Qur'ani Tukufu ambacho kimefanyika hivi karibuni kwa njia ya intaneti, amesema Waislamu kote duniani wanawajibika katika kufanikishwa vikwazo hivyo.
Habari ID: 3477375    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/08/03

Watetezi wa Qur'ani Tukufu
TEHRAN (IQNA) - Msomi wa Malaysia anasema ili kujibu kiuchumi mashambulizi ya Wamagharibi dhidi ya Uislamu na Qur'ani Tukufu, mataifa ya Kiislamu yanahitaji kuelewa uwezo wao na kujenga umoja.
Habari ID: 3477373    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/08/03

Watetezi wa Qur'ani
TEHRAN (IQNA) – Washiriki katika kongamano la kimataifa ambalo limeitishwa kujadili njia za kukabiliana na kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu wamesisitiza haja ya ulimwengu wa Kiislamu kuwa na umoja na mshikamano wa uhakika ili kkukabiliana na vitendo hivyo vya kufuru.
Habari ID: 3477372    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/08/02

Watetezi wa Qur'ani Tukufu
STOCKHOLM (IQNA) - Mwanazuoni wa Kiislamu mwenye makazi yake nchini Uswidi anasema vitendo vya mara kwa mara vya kuvunjiwa heshima Qur'ani katika nchi hiyo ya eneo la Nordic barani Ulaya vinaiweka sura ya Uswidi hatarini.
Habari ID: 3477360    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/30

Watetezi wa Qur'ani Tukufu
TEHRAN (IQNA) – Mwanaharakati wa kisiasa na haki za binadamu wa Bahrain amependekeza kwamba muungano wa taasisi za kiraia katika nchi za Kiislamu na zisizo za Kiislamu uanzishwe ili kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu na kuvunjiwa heshima matakatifu ya Kiislamu.
Habari ID: 3477359    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/30

Mashindano ya Qur'ani
TEHRAN (IQNA) – Hafidh wa Qur'ani Tukufu kutoka Pakistani ambaye anashiriki katika fainali ya Mashindano ya 39 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran amesifu kiwango cha juu cha mashindano hayo.
Habari ID: 3476598    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/02/21

Mwaka wa 44 wa Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) – Warsha ya kimataifa inatazamiwa kufanyika siku ya Jumatano kwa njia ya intaneti kwa lengo la kujadili Mapinduzi ya Kiislamu.
Habari ID: 3476527    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/02/07

Kumbukizi ya Shahidi Soleimani
TEHRAN (IQNA) – Mwanachama mwandamizi wa harakati ya muqawama au mapambano ya Palestina, Jihad Islami, amesema shahidi Qassem Soleimani aliweza kutoa motisha kwa wapiganaji wote wa harakati za mapamano.
Habari ID: 3476351    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/01/03

Uchambuzi wa kisiasa
TEHRAN (IQNA) - Kwa mujibu wa mtaalamu kutoka Ujerumani, mazungumzo kuhusu bei ya nishati na vile vile kutetea uhusiano wa kawaida kati ya Saudi Arabia na utawala wa Israel ni kati ya ajenda ya ziara ya kwanza ya Rais wa Marekani Joe Biden katika eneo la (Asia Magharibi) Mashariki ya Kati.
Habari ID: 3475468    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/07/06

TEHRAN (IQNA)- Kongamano la kimataifa la kujadili mfumo na nidhamu ya pamoja ya majaji wa mashindano ya kimataifa ya Qur’ani limemalizika Alhamisi katika mji wa Karbala nchini Iraq.
Habari ID: 3474834    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/01/21

TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaandaa ramani ya njia ya ushirkiano na nchi zingine kwa kuzingatia maslahi yake ya taifa.
Habari ID: 3474832    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/01/21

TEHRAN (IQNA)- Warsh ya kujadili 'Hali ya Qiraa na Tajwid ya Qur'ani Tukufu Barani Afrika' imepangwa kufanyika wiki ijayo kwa njia ya intaneti.
Habari ID: 3474600    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/11/25

TEHRAN (IQNA) – Jamhuri ya Azerbaijan imewafungia watumizi wa inteneti nchini humo tovuti ya Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa.
Habari ID: 3474473    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/26

TEHRAN (IQNA)- Wanachama kadhaa wa jamii ya Qur'ani nchini Iran, wakiwemo wasomaji wakongwe wa Qur'ani, wanazuoni na wasimamizi wa taasisi za Qur'ani wamekutana Jumamosi katika ofisi za Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) katika siku ya kwanza ya kazi ya mwaka mpya wa 1400 Hijria Shamsiya
Habari ID: 3473780    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/04/04

TEHRAN (IQNA)- Fainali ya kitengo cha wanawake katika Mashindano ya 37 Kimataifa ya Qur’ani ya Iran ilianza Jumapili.
Habari ID: 3473715    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/03/08

TEHRAN (IQNA) – Wiki hii kumefanyika kumbukumbu kwa mwaka mwaka wa 27 tokea Mzayuni mmoja aliyekuwa na misimamo ya kufurutu ada aliwashambulia na kuwamiminia risasi Waislamu waliokuwa wakitekeleza ibada ya Swala katika Msikiti wa Haram ya Nabii Ibrahim mjini al Khalil (Hebron) huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
Habari ID: 3473688    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/28

TEHRAN (IQNA) – Watu wasiopungua sita wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya gaidi kufyatua bomu baada ya swala ya Ijumaa katika msikiti uliooko katika bandari ya Kismayo, kusini mwa Somalia.
Habari ID: 3473159    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/11

TEHRAN (IQNA) – Mkuu wa Akademia ya Elimu, Utamaduni na Utafiti Iran (ACECR) amesema academia hiyo inapaswa kuongoza duniani katika ustawi wa sayansi na teknolojia.
Habari ID: 3473037    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/05