IQNA

Hamu ya kuzuru Haram Takatifu iliyojaa nuru ya Musa bin Ja'afar Al-Kadhim

Imamu wa saba wa Waislamu wa madhehebu ya Shia duniani, ni Imam Musa bin Ja'afar Al-Kadhim (AS) ambaye ana lakabu ya Babul Hawaij, kwa sababu ya watu kutasawali kwa Mwenyezi Mungu Mola Mweza kupitia kwake.

Katika kipindi cha miaka 35 ya Uimamu wake, kuanzia mwaka 148 hadi 183 hijria, Imam Musa Al-Kadhim alikuwa akiwabainishia watu kwa njia na sura tofauti mfumo matulubu wa kisiasa na kijamii wa Uislamu. Kipindi cha maisha ya Imam Musa Kadhim (as) kilisadifiana na tawala za makhalifa kadhaa wa Bani Abbas, zama ambazo uimla na udhalimu wa watawala wa Bani Abbas ulifikia kilele. Baada ya kuuawa shahidi mikononi mwa mamluki wa mtawala Harun Al-Rashid, Uimamu ulimfikia ndugu yake, Imam Ali bin Musa Ridha (AS).

Kishikizo: Imam Musa Kadhim ، waislamu