IQNA

Kiongozi Muadhamu: Vipawa vya vijana vinaweza kuleta ustaarabu mpya wa Kiislamu

TEHRAN (IQNA)- a Iran unaweza kuandaa uwanja wa kujaza mapengo ya kielimu ya nchi na ikawezekana kuvuka mipaka ya kimataifa ya kielimu, na hivyo kuleta ustaarabu mpya wa Kiislamu na kuwa na mustakabali unaong’ara.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema hayo leo alipokutana na vijana wenye vipawa na vipaji vya juu vya kielimu na kubainisha kwamba, taifa la Iran ni taifa lenye kipaji na ndio maana tangu kale limekuwa likiandamwa kwa vita laini vya udhalilishaji vya wakoloni ili kwa njia hiyo lisahau vipawa na uwezo wake wa kielimu na hata likane hilo na hivyo kuamini uongo mkubwa wa “sisi hatuwezi”.

Kiongozi Muadhamu ameongeza kuwa, katika kipindi cha miaka 200 iliyopita ya Iran pia. wakoloni na watawala wa wakati huo wa taifa hili, kwa pamoja walikuwa wakipiga ngoma ya 'kutokuwa na uwezo taifa la Iran" ambapo ushindi wa mapinduzi ya Kiislamu ulikuja kuhitimisha hilo.

Ayatullah Khamenei amebainisha kuwa, mghafala na uporaji ni malengo mawili yanayokamilishana ya wakoloni na kujaribu kueneza fikra ya ‘kutokuwa na uwezo” baina ya mataifa na kuongeza kuwa, wakati taifa fulani linapoghafilika na uwezo wake, uporaji ni jambo ambalo huwezekana kirahisi kabisa.

Akitoa ushahidi wa Aya za Qur’ani zinazototahadharisha kuhusiana na matokeo mabaya ya kughafilika, Ayatullah Khamenei ameeleza kuwa, Mwenyezi Mungu anatahadharisha katika Kitabu cha Mbinguni kwamba, adui anataka mghafilike na silaha na vitu vyenu mlivyonavyo ili aweze kukushambulieni kwa urahisi. 

Kiongozi Muadhamu amekumbusha matamshi yake ya miaka kadhaa iliyopita kuhusiana na mustakabali wa Iran na udharura wa kuweko himaya na uungaji mkono katika uga wa elimu kimataifa na kusema kuwa, tunapaswa kufanya mambo kwa namna ambayo katika mustakabali unaokubalika kiakili Iran iwe chanzo cha elimu kimataifa na mtu ambaye atataka kupata kitu kipya cha kielimu alazimike kujifunza lugha ya Kifarsi kama ambavyo katika zama fulani, Iran ilikuwa katika vilele vya elimu kimataifa na vitabu vya wasomi wa Kiirani vilikuwa vikifundishwa  katika Vyuo Vikuu vya Magharibi na Mashariki na marejeo ya wasomi.

4013976