IQNA

Kisomo cha Mbinguni: Msikilize Sheikh Abdul Basit Abdul Samad akisoma aya za Qur'ani za Surah Maryam

IQNA – Kinachofuata ni qiraa au usomaji wa aya za 33-35 za Surah Maryam na qari maarufu wa Misri marhum Sheikh Abdul Basit Abdul Samad.
 

Na amani iko juu yangu siku niliyo zaliwa, na siku nitakayo kufa, na siku nitakayo fufuliwa kuwa hai.

Huyo ndiye Isa mwana wa Maryamu. Ndiyo kauli ya haki ambayo wanaifanyia shaka.

Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwa na mwana, Subhanahu, Yeye ametakasika! Anapo lihukumia jambo basi huliambia tu: Kuwa! Likawa.

 

Mtume Muhammad (SAW) alisema wakati mmoja kwamba kuisikiliza Qur'ani Tukufu humletea mja thawabu za Mwenyezi Mungu, huku kila herufi ikisikika ikistahiki tendo jema kwa msikilizaji, na kumpandisha msikilizaji katika safu ya wale wanaosoma maandiko matukufu na kupaa kuelekea mbinguni. 
Shirika la habari la IQNA limeratibu na kutoa mfululizo unaoitwa "Kisomo cha Mbinguni," wenye kumbukumbu za kuvutia za wasomaji maarufu Qur’ani Tukufu.

Kishikizo: sura maryam ، isa bin maryam