IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu /19

Sura Maryam; Kisa cha Mama Mwema aliyetakasika

12:41 - July 21, 2022
Habari ID: 3475521
TEHRAN (IQNA) – Bibi Maryam, mama yake Nabii Isa (AS), ametajwa ndani ya Qur'ani Tukufu kuwa ni mwanamke mwema aliyetakasika, ambaye hakuwa mtume bali alilelewa kama nabii na ambaye mwenendo wake ulikuwa kama ule wa Mitume wa Mwenyezi Mungu.

Sura Maryam ni sura ya 19 ya Qur'ani Tukufu ambayo ina aya 98 na iko katika  Juzuu ya 16. Ni sura ya Makki (imeteremshwa Makka) na ni Sura ya 44 iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume (SAW).

Aya ya 16 hadi 27 na aya ya 34 ya Sura inasimulia kisa cha maisha ya Bibi Maryam (AS) na kwa hiyo imepewa jina la mwanamke huyo aliyetakasika.

Surah Maryam ina sifa mbili maalum: Kwanza, kuna neno Udhkur (kumbuka) wakati wa kusimulia hadithi za manabii wakubwa, na pili, neno Rahman (Mwenye Huruma), ambalo ni moja ya sifa za Mwenyezi Mungu, limetajwa katika Sura hii mara 16 , huku baadhi ya wafasirina wakisema wakisema inaonyesha rehema na huruma ya Mwenyezi Mungu kwa wote, hasa kwa manabii na waaminifu.

Katika ufafanuzi ulioko katika tafisri yake ya  Al-Mizan ya Qur'ani Tukufu, Allamah Tabatabaei anarejelea Indhar (onyo) na Bisharat (habari njema) kama ujumbe mkuu wa Sura ambao umeelezwa katika hadithi za Mitume.

Sura hii imewagawanya watu katika makundi matatu: Wale ambao ni miongoni mwa wapokezi wa neema za Mwenyezi Mungu, wakiwemo manabii na walioongoka, waliotubu na waaminio waliotenda mema, na waliopotea na ni maswahaba wa Shetani.

Sehemu kuu ya Sura inasimulia kisa cha Zakariya , Maryam, Isa, Yahya , Ibrahim na mwanawe Ismail, Idris na baadhi ya mitume wengine wa Mwenyezi Mungu.

Sehemu ya kwanza ya Sura inataja kisa cha Zakariya ambacho kinafanana na kile kinachotajwa katika Injili ya Luka ya Bibilia. Pia inamuashiria Bibi Maryam-Amani ya Mwenyezi Mungu Iwe Juu Yake- (SA) kupata mimba, na kisha kuzaliwa Nabi Isa au Yesu –Amani ya Mwenyezi Mungu Iwe Juu Yake-(AS) na kuzungumza kwake akiwa yungali mchanga katika susu, kusifu ukweli wake na pia  Ikhlas (usafi wa nia) yake.

Maryam, mama yake Isa, ni miongoni mwa wanawake wanaoheshimika miongoni mwa Waislamu. Mwenyezi Mungu alimfanya kuwa msafi na akamchagua kutoka miongoni mwa wanawake wote. Isa  (AS) alishuhudia usafi na wema  wa mama yake akiwa angali mtoto mchanga. “(Mtoto) akasema: Hakika mimi ni mtumwa wa Mwenyezi Mungu. Amenipa Kitabu, na amenifanya Nabii. Na amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo. Na ameniusia Sala na Zaka maadamu ni hai, Na nimtendee wema mama yangu. Wala hakunifanya niwe jeuri, mwovu. Na amani iko juu yangu siku niliyo zaliwa, na siku nitakayo kufa, na siku nitakayo fufuliwa kuwa hai." ( Aya ya 30-33 ).

Habari zinazohusiana
captcha