IQNA

Wito wa kutuma athari katika Kongamano la Kimataifa la Ali Asghar (AS)

10:34 - November 02, 2010
Habari ID: 2023849
Kongamano la Kimataifa la kumuenzi Ali Asghar (AS) linatazamiwa kufanyika nchini Iran na wanaotaka kushiriki wameombwa watume athari na kazi zao za kisanaa katika nyanja mbalimbali.
Katika mahojiano na IQNA, Bw. Parviz Eskandarpur Khurmi Mkuu wa Kamati ya Kiutamaduni na Kisanaa ya Kongamano la Kimataifa la Kumuenzi Ali Asghar (AS) amesema athari hizo zinapaswa kuashirikia madhumuni ya matukio ya Ashura na Karbala na nafasi ya Ali Asghar (AS) katika matukio hayo. Amesema athari hizo zinaweza kujumuisha nakshi, michoro, taswira, kaligrafia, picha, filamu fupi na animation, michoro ya watoto, mashairi na makala.
Ali Asghar alikuwa mtoto wa mwisho wa mjukuu wa Mtume (SAW), Imam Hussein (AS). Katika riwaya imesimuliwa kuwa katika mapambano ya Karbala wakati Imam Hussein (AS) alipopaza sauti na kusema Je, yuko yeyote wa kutusaidia?, yuko yeyote wa kutuitikia na kututimizia haja yetu?, mwito huu haukuitikiwa na yeyote ila mtoto mchanga Ali Asghar bin Hussein ambae alikuwa na umri wa miezi sita tu. Mtoto huyo aliangua kilio kama ishara ya kuitikia mwito wa baba yake. Imam Hussein (AS) alimbeba mtoto huyu mchanga aliyekuwa akipapatika mikononi mwake kwa kiu ya maji. Mtoto huyo mchanga hakuweza kustahamili dhiki, na hivyo Imam Hussein (AS) alitoka nae nje lakini aah... maadui walimjibu kwa kumpgaAli Asghar kwa mshale wa vyembe vitatu na akafa shahidi mikononi mwa baba yake.
Imam Hussein (AS) alirudi katika hema lake na mwili wa mtoto mikononi mwake. Imam Hussein hatimae alimchimbia kaburi dogo kwa upanga wake na kumzika mtoto huyo.
683122
captcha