IQNA

Qiraa ya Qur'ani

Qari maarufu wa Bangladesh akisoma Surah Al-Infitar kwenye kipindi cha TV cha Mahfel (+Video)

16:09 - April 13, 2024
Habari ID: 3478678
IQNA – Sheikh-ul-Qurra (mbora wa maqari) wa Bangladesh ni miongoni mwa maqari ambao qiraa yake imevutia wengi katika cha Televisheni cha Mahfel.

Sheikh Ahmed Yusuf al-Azhari alisoma Aya ya 13 hadi 19 ya Surah Al-Infitar katika kipindi hicho.

Hakika wema bila ya shaka watakuwa katika neema,  Na hakika waovu bila ya shaka watakuwa Motoni; . Wataingia humo Siku ya Malipo.  Na hawatoacha kuwamo humo.  Na nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani?  Tena nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani?  Siku ambayo nafsi haitakuwa na madaraka yoyote juu ya nafsi; na amri yote siku hiyo ni ya Mwenyezi Mungu tu.

Kipindi cha Televisheni cha Mahfel kilikuwa kipindi maalumui cha Qur'ani kilichorushwa hewani na kanali ya tatu ya televisheni ya Shirika la Utangazaji wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Kipindi hicho maarufu kilirushwa katika  chaneli ya 3 ya IRIB  katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Kipindi hicho, ambacho mwaka huu kilikuwa msimu wa pili, kilikuwa kikitangazwa kabla ya Magharibi kila siku katika mwezi mtukufu, na kuwapa watazamaji hali nzuri ya kiroho wanapojitayarisha kufuturu. 

Kwa kuzingatia Qur'ani, kindi hiki kinalenga kuwapa watu waliofunga muda mfupi wa kunufaika na  mijadala yenye utambuzi na usomaji wenye kuvutia wa Qur'ani Tukufu.

4209964

captcha