IQNA

Mafundisho ya Kiislamu

Fatwa Milioni 1.5 hutolewa katika lugha 12 nchini Misri kila mwaka

17:48 - April 17, 2024
Habari ID: 3478693
IQNA - Kituo cha Darul Iftaa cha Misri kimetoa Fatwa milioni 1.5 mshauri wa Mufti Mkuu wa nchi hiyo alisema.

Sheikh Ibrahim Najm, ambaye pia anahudumu kama katibu mkuu wa Baraza la Fatwa Ulimwenguni, aliongeza kuwa Fatwa hizo hutolewa kwa lugha 12, gazeti la al-Watan iliripoti.

Ameyasema hayo alipokuwa akihutubia mkutano wa kimataifa kuhusu kupambana na itikadi kali na ugaidi.

Mkutano huo unaendelea nchini Singapore kuanzia Aprili 13 hadi 18 kwa kushirikisha nchi 40.

Najm alisisitiza zaidi jukumu la Baraza la Fatwa Ulimwenguni katika kutoa Fatwa, akisema mtazamo wa baraza hilo unategemea misimamo ya  wastani.

Kwingineko katika maelezo yake, Sheikh Najm alisisitiza haja ya kuanzisha kituo cha kufanya utafiti kuhusu misimamo mikali ili kukabiliana vyema na mawazo ya itikadi kali na kuendeleza amani.

Aidha amevitaka vyombo vya habari na serikali kuwa makini zaidi katika kuwashughulikia wasomi wa dini. Aliendelea kusema kwamba dini ya kweli ina uwezo wa kutoa suluhu kwa changamoto zinazoukabili ulimwengu.

3487975

captcha