IQNA

Hija na Umrah

Kikao cha Madina kujadili fursa za kuboresha Hija ya Umra

11:02 - April 18, 2024
Habari ID: 3478698
IQNA – Kikao cha kwanza cha Jukwaa la Hija na Umrah kimepangwa kuanza Jumatatu ijayo, Aprili 22, katika mji mtakatifu wa Madina, Saudi Arabia.

Kongamano hilo litafanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mfalme Salman kwa lengo la kuimarisha utekelezaji wa ibada za Hija na Umrah (Hija Ndogo) na kuandaa mazingira sahali ya kuzuri miji mitakatifu ya Makka na Madina, ili kuongeza hali ya kuridhika miongoni mwa Mahujaji.

Hafla hiyo itahusisha ushirikiano na Mpango wa Huduma ya Mahujaji na inajumuisha ushiriki kutoka kwa wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na maafisa wa serikali, watoa huduma wa sekta binafsi kuanzia sekta ya usafiri,  bima, afya, makazi na malazi, mawasiliano ya simu n.k

Mbali na vikao vya mawasilisho na warsha, kongamano hilo litajumuisha maonyesho yanayoonyesha huduma mpya na bidhaa za ubunifu zinazolenga kuboresha tajriba ya hija. Wizara ya Hijja na Umrah ya Saudi pia itatangaza fursa mpya na ushirikiano unaolenga kuwezesha na kuimarisha safari katika miji mitakatifu.

Kishikizo: hija umra makka madina
captcha