IQNA

Qur'ani Tukufu

Mtafiti: Kusimulia hadithi ni njia muhimu ya kisanaa ya kueneza mafundisho ya Qur'ani

16:46 - April 13, 2024
Habari ID: 3478680
IQNA - Mtafiti wa Guinea-Bissau anasema mbinu ya kusimulia hadithi imetumika katika Qur'an na inaweza kueneza mafundisho ya Kiislamu kwa ufanisi.

Mtafiti: Kusimulia hadithi ni njia muhimu ya kisanaa ya kueneza mafundisho ya Qur'ani

IQNA - Mtafiti wa Guinea-Bissau anasema mbinu ya kusimulia hadithi imetumika katika Qur'an na inaweza kueneza mafundisho ya Kiislamu kwa ufanisi.

Musa Debu, mtafiti na PhD mgombea katika Chuo Kikuu cha Al Mustafa aliiambia IQNA: "Qur'ani Tukufu hutumia hadithi au visa vya manabii kuwasilisha ujumbe wake kwa njia nzuri sana, na kufanya usimulizi wa hadithi kuwa nyenzo muhimu ya kisanaa ya kueneza mafundisho yake,"

"Ninaamini kusimulia visa au hadithi ni muhimu sana katika kueleza ujumbe wa Uislamu kwa njia ya sanaa kwani Qur'ani yenyewe inasimulia matukio mbalimbali, yakiwemo maisha ya mitume na matukio ya kufurahisha na ya kusikitisha," alisema.

Dabu ambaye anasema ameihifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu aliongeza kuwa: "Kwa kusimulia hadithi hizi za Qur'ani, tunaweza kuwakumbusha watu kuhusu darsa zilizomo."

Pia aliashiria ushawishi mkubwa ambao hadithi za maisha ya Ahlul-Bayt (AS) na namna ambavyo zinaweza kuwa nazo kwa watu binafsi.

"Ubinadamu unaweza kuepuka dhulma na kiburi kwa kufuata kikamilifu mafundisho ya Qur'ani," alisisitiza, akiashiria umuhimu wa matukio makubwa ya Qur'ani kama Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran ambayo yamefanyika katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

"Ili kuwakomboa watu kutokana na dhulma na kiburi, kama alivyofanya Mtukufu Mtume (SAW), ni lazima wanadamu warejee kwenye Qur'ani," alisema, huku akinukuu aya ya Qur'ani: "Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni nalo.” (Surah Al-Imran, aya ya 103).

Toleo la 31 la Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran lilifikia tamati tarehe 2 Aprili baada ya wiki mbili. Sehemu ya kimataifa ilishirikisha wawakilishi kutoka nchi 25, wakionyesha michango yao ya Qur'ani.

Maonyesho hayo huandaliwa kila mwaka na Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. Hulenga kukuza ufahamu Qur'ani na kuendeleza shughuli za Qur'ani.

 4209714

 

Kishikizo: qurani tukufu guinea
captcha