IQNA

Mashindano ya Qur'ani Algeria

Algeria kuongeza zawadi za fedha taslimu katika mashindano ya Qur'ani

14:45 - April 14, 2024
Habari ID: 3478682
IQNA - Rais wa Algeria ameamuru kuongezwa kwa zawadi za fedha zinazotolewa kwa washindi wa mashindano ya Qur'ani nchini humo.

Abdelmadjid Tebboune alitoa amri, ya kuamuru kupanda kwa thamani ya zawadi za fedha taslimu katika mashindano ya kitaifa na kimataifa ya Qur'ani ya Algeria, TV ya Algeria iliripoti.

Kulingana na amri hiyo, washindi wa nafasi tatu za juu katika mashindano ya kimataifa watapata dinari milioni 325, dinari milioni 250 na dinari milioni 150 za Algeria, mtawaliwa.

Pia, watakaoshika nafasi ya kwanza hadi ya tatu katika hafla ya kitaifa ya Qur'ani watatunukiwa dinari milioni 100, milioni 75 na milioni 50.

Rais wa Algeria pia aliamuru mashindano ya Qur'ani kwa watoto yafanyike nchini humo huku washindi wakipokea zawadi za fedha taslimu kati ya dinari milioni 50 hadi 100 milioni.

Katika miaka ya hivi karibuni, Algeria imeshuhudia ongezeko kubwa la shughuli za Qur'ani, ikiwa ni pamoja na mashindano ya Qur'ani katika ngazi tofauti.

Algeria ni nchi iliyoko Afrika Kaskazini. Waislamu ni takriban asilimia tisini na tisa ya wakazi wa nchi hiyo.

3487924

Kishikizo: algeria qurani tukufu
captcha