IQNA

Wanaharakati wa kike wa Qur’ani Iran waenziwa

8:14 - July 04, 2011
Habari ID: 2148315
Pembizoni mwa Mashindano ya 28 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Iran wanawake 28 wanaharakati wa Qur’ani wameenziwa Julai pili katika sherehe iliyoandaliwa na Shirika la Awqaf la Iran.
Hafla hiyo imehudhuriwa na Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami, mwanachama mwandamizi wa Baraza la Wataalamu la Iran.
Bi. Maasoumeh Farzaneh amewasilisha ripoti kuhusu harakati za Qur’ani za Idara ya Wanawake katika Shirika la Awqaf la Iran.
Katika hotuba yake Mkuu wa Shirika la Awqaf la Iran Hujjatul Islam Ali Muhammadi amesema kuwa: ‘Wanawake wanaofuata Qur’ani huwa wamelelewa na akina mama wanaofuata Qur’ani. Tuna fahari kuwa na wanawake wacha Mungu katika jamii ambao wamefanikiwa katika uga wa kimataifa’ amesisitiza Ali Muhammadi.
Naye Ayatullah Ahmad Khatami amesema: ‘Moja ya mafanikio ya Mapinduzi ya Kiislamu ni kuwepo maelfu ya maqarii na mahufadh wa Qur'ani Tukufu wanawake na wanaume katika uga wa kitaifa na kimataifa’. Amesema kuna haja ya kuzingatiwa tafsiri ya Qur'ani sambamba na kuhifadhi na kusoma kitabu hicho ktukufu’. Ameongeza kuwa Bibi Fatima Zahra SA alikuwa mtaalamu wa kwanza wa Qur’ani na kuongeza kuwa, mtaalamu halisi wa Qur’ani ni yule anayetekeleza mafundisho yake ipasavyo.
Kati ya wanawake walioenziwa ni pamoja na Roqayyeh Harati, Tahereh Mohseni, Nafiseh Kabiri, Susan Bani Ali, Azedeh Haji Gholami, Ashraf Basiri, Zahra Azizpuriyan, Seyyedeh Mona Salehi, Ghezbast Ahadpur, Zahra Jahanpur, Dr. Abdulbaghi, Hejazidust, Nankoli, Qaravi, Kalantari, Kashani Wahid, Abbasi Nazari, Moghaddasi, Abdoli, Husseinifar, Jabini, Ja’fari, Khatami, Zahra Ja’fari na Farideh Jalali.
818604
captcha