Wakaazi wa Sarajevo wawaaga mashahidi wa Srebrenica
Mamia ya wakaazi wa mji mkuu wa Bosnia na Herzegovina wameshiriki katika mazishi ya watu 127, waliouawa katika mauaji ya umati ya Waislamu wa mji wa Srebrenica mwaka 1995, ambao miili yao imepatikana hivi karibuni katika kaburi la umati.