IQNA

Wanachama wa ACECR watangaza upya ahadi ya utiifu kwa Misingi ya Imam Khomeini

IQNA – Maafisa na wafanyakazi wa Akademia ya Elimu, Utamaduni na Utafiti Iran (ACECR) siku ya Jumapili, Februari 8, 2026, walitembelea kaburi la Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu Amrehemu) kusini mwa mji wa Tehran.

Ziara hiyo, iliyofanyika mkesha wa maadhimisho ya miaka 47 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, ilikuwa ni fursa ya kutoa heshima kwa marehemu mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kufanya upya bay’ah (ahadi ya utii wa kimaadili) kwa misingi na fikra zake.

Washiriki walisisitiza mshikamano wao na urithi wa Imam Khomeini (RA), urithi unaojengwa juu ya uadilifu, uhuru, na kujitolea kwa thamani za Kiislamu, wakisisitiza dhamira ya kuendeleza malengo ya Mapinduzi ya Kiislamu katika nyanja za elimu, utamaduni na utafiti kwa maslahi ya jamii na Umma kwa ujumla.