IQNA

Mashindano ya Sita ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Wanafunzi Waislamu katika vyuo vikuu yamemalizika Jumapili katika mji wa Mashhad, kaskazini mashariki mwa Iran kwa kuzawadiwa washindi wa kategopria za qiraa na kuhifadhi Qur'ani Tukufu. Mashindano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Kiutamaduni wa Nur.