IQNA

Mvuto wa Hormozgan Umeangaziwa Katika Matukio ya ‘Iran-e Jaan’

IQNA – Mradi wa “Iran-e Jaan” uneendeshwa na Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) kwa lengo la kuonesha mikoa ya Iran zaidi kwenye televisheni za kitaifa na kimataifa za shirika hilo

Hormozgan ni mkoa wa saba kuzingatiwa katika mradi huu, ambapo mipango mbalimbali na matukio yanatekelezwa kwa kaulimbiu ya “Hormozgan; Hadithi ya Ardhi Yenye Fursa za Bahari.”

Mkoa wa Hormozgan ni mmoja kati ya mikoa 31 ya Iran. Mji wake mkuu ni Bandar Abbas. Mkoa huu uko kusini mwa nchi, ukipakana na Oman na Umoja wa Falme za Kiarabu.