IQNA

Msikiti wa Kufa ni miongoni mwa misikiti minne mikubwa zaidi duniani na uko kilomita 12 kaskazini mwa mji wa Najaf nchini Iraq.

Msikiti huu ni wa nne kwa umuhimu kwa Waislamu wa madhehebu ya Shia baada Masjid al Haram, Al Masjid an Nabawi na Masjid al Aqsa. Msikiti wa Kufa uliasisiwa na Nabii Adam AS na katika kipindi chote cha historia ulitumiwa na manabii na mawalii wa Mwenyezi Mungu SWT ikiwa ni pamoja na Mtume Muhammad SAW, Amir ul Muminin Ali AS, Imam Hassan AS, Imam Hussein AS na Maimamu wengine watoharifu. Pembizoni mwa jengo la kihisitoria la msikiti huo palikuwa na nyumba ya Imam Ali AS , Dar al Imara ya Kufa, Haram Takatifu za Maitham Tammar, Muslim bin Aqil, Hani bin Urwa na Mukhtar Thaqafi.