IQNA

Nyumba ya Shahidi Chamran

Shahidi Chamran Save'e alizaliwa Oktoba Pili 1932 mjini Tehran na aliuawa shahidi Juni 21 1982 katika eneo la Dehlavieh akiwa katika medani ya vita vya Iraq dhidi ya Iran.

Alikuwa mwanafizikia, waziri wa ulinzi katika serikali ya Mahdi Bazargan na serikali ya muda ya Baraza la Mapinduzi. Akiwa pamoja na Imam Musa Sadr waliunda Harakati ya Amal nchini Lebanon, aliwahi kuwa mbunge katika duru ya kwanza ya Bunge la Iran, Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, na alikuwa miongoni mwa makamanda wa Iran katika vita vya kulazimishwa vya Iraq dhidi ya Iran. Aidha alikuwa mwanzilishi wa kamandi ya vita visivyo vya kawaida katika vita vya Iraq dhidi ya Iran. Mwaka 2008 Manispaa ya Tehran iliikarabati nyumba ya Shahidi Chamran na kuifanya kuwa jengo la makumbusho.