IQNA

Kikao cha kujadili 'Nukta za Muamala wa Karne' ambao ni njama ya pamoja ya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel kilifanyika Julai 8 katika makao makuu ya Shirika la Habari la Qur'ani la Kimataifa, IQNA. Kikao hicho kilihudhuriwa na Balozi wa Palestina nchini Iran Salah al-Zawawi pamoja Hussein Sheikhul Islam, mwanadiplomasia mkongwe wa Iran ambaye pia ni mshauri wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu.