IQNA

Mji wa Madina uko kaskazini mwa Riyadh, mji mkuu wa Saudi Arabia kati kati mwa Najd na ni mji wenye hali ya hewa kavu na joto kali na pia baridi kali wakati wa msimu wa baridi. Jina la mji huo lilikuwa ni Yathrib kabla ya Hijra ya Mtume Muhammad SAW na ulijulikana kama Madina al Nabii (Mji wa wa Nabii) baada ya kuwasili Mtume Muhammad SAW. Msikiti wa Mtume, Al-Masjid an-Nabawi, Msikiti wa Quba na Msikiti wa Qibalatian ni misikiti muhimu iliyo katika mji huo. Mji wa Madina ni kati ya miji mitakatifu kwa Waislamu na kaburi la Bwana wetu Mtume Muhammad SAWA liko katika , Al-Masjid an-Nabawi na hivyo eneo hilo ni kati ya maeneo matakatifu zaidi kwa Waislamu duniani.