IQNA

Maandamano India kupinga sheria ya uraia kabla ya safari ya Trump

Maandamano makubwa yalifanyika katika mji wa New Delhi India kabla ya Rais Donald Trump wa Marekani kuwasili nchini humo Jumapili. Ghasia ziliibuka katika maandamano ya kupinga sheria hiyo ambayo wakosoaji wanasema inalenga kuwakandamiza na kuwadhoofisha Waislamu nchini humo.