IQNA

Katika siku hizi za karantini na watu kuhimizwa kukaa nyumbani katika maeneo mbali mbali duniani ili kukabiliana na ugonjwa wa corona, vijana Wapalestina wenye kujitolewa huko Ghaza wanasambaaza vitabu na vifaa vya masomo miongoni mwa watoto Wapalestina wanaoishi katika kambi ya Deir al Balh kusini mwa Ukanda wa Ghaza.

Zawadi hizo zimeweza kuleta furaha kwa watoto hao ambao wana wakati mwingi katika kipindi hiki cha corona.