IQNA

Katika hali ambayo janga la corona au COVID-19 limepelekea Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka huu utafautiane na miaka iliyopita. Pamoja na kuwepo vizingiti vilivyowekwa kuzuia kuenea ugonjwa huo, Waislamu kote duniani wameendelea kutekeleza mijimuiko ya kidini na ibada za mwezi huu mtukufu kwa kuzingatia kanuni za afya.