IQNA

Umoja wa Falme za Kiarabu ni kati ya nchi za ukanda wa Ghuba ya Uajemi. Nchi hii inakadiriwa kuwa na misikiti 4,818 na miongoni mwa misikiti hiyo imo iliyo mmaridadi zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu.

Kwa mujibu wa takwimu rasmi kuna misikiti 1,418 Dubai, misikiti 2,289 katika mji mkuu Abu Dhabi na misikiti 600 katika mji wa Sharjah.