IQNA

Watu wa Uturuki washerehekea Hagia Sophia kurejea katika hadhi ya msikiti

TEHRAN (IQNA) – Wanaharakati na waumini wamekusanyika nje ya Hagia Sophia mjini Istanbul, Uturuki kusherehekea kugeuzwa jengo hilo kuwa msikiti na baada ya kuwa jumba la makumbusho kwa muda mrefu.

Mahakama ya Kilele ya Uturuki imeafiki kufuta uamuzi wa serikali wa tangu mwaka 1934 ambao ulilipatia jumba la Hagia Sophia huko Istanbul hadhi ya jumba la makumbusho.

Huku wakitamka nara ya Allahu Akbar, waliokusanyika hapo walisikia kwa furaha Adhana katika Msikiti wa Hagia Sophia.

 

 
 
Kishikizo: Hagia Sophia ، Uturuki