Sherehe za kufunga mashindano hayo zilifanyika katika ikulu ya rais mjini Ankara Jumatano usiku na kuhudhuriwa na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.
Washindi wa kategoria hizo mbili, yaani kusoma Qur'ani na kuhifadhi Qur'ani Tukufu walitunukiwa zawadi na kupewa vyeti vya heshima na Rais Erdogan katika sherehe hizo.
Katika qiraa ya Qur'ani Tukufu, qari kutoka wa nchi mwenyeji alishinda tuzo ya juu. Seyed Parsa Angoshtan kutoka Iran aliibuka wa pili na mwakilishi wa Afghanistan akaibuka wa tatu.
Katika kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu , Milad Asheghi wa Iran alimaliza wa pili huku wahifadhi kutoka Bangladesh na Malaysia wakishinda nafasi za kwanza na ya tatu kwa utaratibu.
Mashindano hayo yalifanyika kwa raundi mbili. Katika duru ya awali, iliyofanyika mwezi Juni, wawakilishi wa nchi 93 waliwasilisha video zilizorekodiwa za usomaji wao kwa kamati ya maandalizi. Baada ya tathmini ya wataalamu, wawakilishi kutoka nchi 47 walifanikiwa kuingia fainali iliyofanyika katika jiji la Sanliurfa kuanzia Oktoba 23-30.
Wataalamu wanne wa Qur'ani kutoka Uturuki na mmoja kutoka Malaysia, Morocco, Kuwait, Lebanon, Jordan na Sudan waliunda jopo la majaji.
3490502