IQNA

Sauti ya kuvutia ya adhana ya Sayyid Muhammad Darchei + Video

TEHRAN (IQNA)- Hujjatul Islam Sayyid Muhammad Javad Mousavi Darchei, qarii na mwalimu wa Qur’ani nchini Iran akiwa safarini nchini Syria alitembelea kaburi la Bilal Habashi , Radhi za Mwenyezi Mungu Ziwe Juu Yake, na akiwa hapo akapata taufiki ya kuadhini.

Bilal Habashi alikuwa muadhini wa Mtume Muhammad SAW  mbali na kuwa sahaba mtiifu na muaminifu wa Mtukufu huyo.

Kaburi la Bilal Habashi liko katika makaburi ya Bab al Saghir mjini Damascus, Syria.

3998226

Kishikizo: bilal habashi ، syria ، muadhini ، darchei