IQNA – Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini nchini Syria imekanusha taarifa zilizosambaa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari kuwa Haram takatifu ya Bibi Zaynab (Salamullahi ‘alayha) mjini Damascus imefungwa.
Habari ID: 3480869 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/29
IQNA – Khatibu wa Swala ya Ijumaa jijini Baghdad amesisitiza umuhimu wa kuwachukulia hatua kali waliotekeleza shambulizi dhidi ya ofisi ya Ayatullah Ali Sistani mjini Damascus, mji mkuu wa Syria.
Habari ID: 3480801 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/07
IQNA – Wizara ya Wakfu ya Syria imeandaa mashindano ya kwanza nchini humo ya kukamilisha usomaji wa Qur’ani nzima kwa siku moja, yakivutia mamia ya wahifadhi wa kiume na wa kike katika misikiti mitatu mikubwa kwenye mji mkuu.
Habari ID: 3480723 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/23
Taarifa
IQNA-Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la nchini Iran (IRGC) limetoa taarifa na kutangaza kuwa kambi ya Muqawama, hususan wanamapambano shupavu na mashujaa wa Palestina, hatimaye itamaliza na kuyakatisha maisha ya aibu ya utawala wa Kizayuni wa Israel ambao unakaliwa ardhi za Palestina kwa mabavu.
Habari ID: 3480490 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/04/04
Muqawama
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesifu na kukutaja kuwa ni kwa kipekee kujitolea kwa kamanda mkuu wa Iran wa kupambana na ugaidi, Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, ambaye aliuawa mwaka 2020 akiwa pamoja na wanajihadi wenzake katika shambulio la kigaidi la ndege isiyo na rubani ya Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad nchini Iraq.
Habari ID: 3479986 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/01/01
Hali ya Syria
IQNA – Wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 13 nchini Syria, Wakristo walibaki waaminifu kwa serikali ya Bashar al-Assad. Lakini kunyakua madaraka kwa kasi kwa kundi la Hay’at Tahrir al-Sham (HTS) kumeongeza wasiwasi kuhusu hatima ya Wakristo walio wachache \ nchini humo.
Habari ID: 3479965 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/12/28
Hali Nchini Syria
IQNA – Kinara wa kundi la Hay’at Tahrir al-Sham (HTS), ambalo limenyakua Madaraka Syria, ameripotiwa kutoa maagizo juu ya kulinda Haram Tukufu ya Baibi Zainab (SA) karibu na mju mkuu Damascus.
Habari ID: 3479939 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/12/22
Muqawama
IQNA-Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei anasema kilichotokea nchini Syria ni "njama ya pamoja ya Marekani na utawala wa Kizayuni", ingawa nchi jirani pia ilishiriki.
Habari ID: 3479892 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/12/11
Uchambuzi
IQNA - Mjumbe wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu wa Iran ametaja sababu nne ambazo anaamini zilisababisha kuanguka kwa serikali ya Bashar al-Assad nchini Syria.
Habari ID: 3479888 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/12/10
Jinai za Israel
IQNA - Milipuko iliyosikika Jumatatu usiku karibu na madhabahu takatifu ya Hadhrat Zeynab (SA) katika kitongoji cha Damascus ilisababishwa na shambulio la bomu la ndege za kivita za Israel, duru zilisema.
Habari ID: 3479887 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/12/10
IQNA - Makundi ya wapiganaji nchini Syria yamepora kaburi takatifu la Hadhrat Zeynab (SA) katika kitongoji cha Damascus nchini Syria, kulingana na picha zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.
Habari ID: 3479881 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/12/09
Diplomasia
IQNA-Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran imesisitiza kuwa, kuainishwa hatima na kufanya maamuzi kuhusu mustakbali wa Syria ni jukumu la pekee la wananchi wa nchi hiyo bila ya uingiliaji uharibifu wala kulazimishwa na mataifa ya kigeni.
Habari ID: 3479879 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/12/09
Matukio
IQNA-Serikali ya Syria ilianguka mapema Jumapili katika mwisho wa kushangaza kwa uongozi wa miaka 24 wa Rais Bashar al-Assad katika nchi hiyo ya Kiarabu baada ya kundi la wanamgambo wa Hay’at Tahrir al-Sham (HTS) kuvamia na kuuteka mji mkuu Damascus.
Habari ID: 3479874 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/12/08
Uchambuzi
IQNA - Utawala wa Kizayuni wa Israel unalenga kwa nguvu zote kusambaratisha mhimili wa muqawama Asia Magharibi na kutenganisha makundi ya muqawama huko Iraq, Syria na Lebanon, amesema mchambuzi wa masuala ya kisiasa wa Iraq.
Habari ID: 3479870 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/12/07
Aragchi katika mkutano na Rais Assad
IQNA-Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza katika mazungumzo yake na Rais Bashar al-Assad wa Syria mjini Damascus, kwamba matukio ya Syria ni sehemu ya njama za utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani dhidi ya eneo la Asia Magharibi.
Habari ID: 3479844 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/12/02
Diplomasia ya Kiislamu
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, muqawama ni utambulisho mzuri na bora wa Syria na akaeleza kwamba, nafasi maalumu iliyonayo Syria katika eneo ni kutokana na utambulisho huu na sifa hiyo muhimu inapaswa kuhifadhiwa.
Habari ID: 3478904 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/05/30
Ahadi ya Kweli
IQNA-Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema iwapo utawala wa Kizayuni wa Israel utafanya harakati yoyote ya kifidhuli utakabiliwa na jibu madhubuti, zito na kali zaidi.
Habari ID: 3478685 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/14
Ahadi ya Kweli
IQNA- Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) limefanya mashambulizi makubwa ya kulipiza kisasi kwa kutumia makombora na ndege zisizo na rubani na makombora dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel likijibu mashambulizi ya kigaidi yaliyofanywa utawala wa Israel ya tarehe 1 Aprili dhidi ya majengo ya kidiplomasia ya Jamhuri ya Kiislamu katika mji mkuu wa Syria, Damascus.
Habari ID: 3478681 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/14
Sikukuu ya Idul Fitr
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei anasema utawala wa Kizayuni wa Israel "lazima uadhibiwe na kutiwa adabu" kwa shambulio lake baya dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran katika mji mkuu wa Syria, Damascus.
Habari ID: 3478662 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/10
Mrengo wa Muqawam
IQNA- Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrallah amesema, haki ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya kutoa jibu kwa uchokozi uliofanywa na utawala wa Kizayuni wa kushambulia ubalozi wake mdogo mjini Damascus ni haki yenye uhalali wa kisheria.
Habari ID: 3478656 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/09