IQNA

TEHRAN (IQNA)- Mtume Muhammad SAW alianza kupokea Wahyi akiwa na umri wa miaka 40 na baada ya miaka 13 ya kuhubiri Uislamu miongoni mwa watu wa Makka, aligura na kuelekea Madina kufuatia mashinikizo ya maadui.

Mtume Muhammad SAW aliaga dunia tarehe 28 mwezi wa Safar mwaka 11 Hijria sasa wa 232 Miladia. Mtukufu huyo alianzisha serikali ya kwanza ya Kiislamu katika mji wa Madina.