IQNA

Nakala kubwa zaidi ya Qur'ani duniani katika maonyesho Dubai

TEHRAN (IQNA)- Sehemu ya nakala ya Qur'ani Tukufu inayotajwa kuwa kubwa zaidi duniani imewekwa katika maonyesho ya Dubai 2020 nchini Umoja wa Falme za Kiarabu.

Nakala hii ya Qur'ani yenye ukubwa wa zaidi ya mita tano mraba inasemekana kuwa yamakini ikawa kubwa zaidi duniani.

Mradi huu ni wa Shahid Rassam, mchongaji mwenye uraia pacha wa Pakistan na Canada ambaye ametumia zaidi ya miaka mitano kuandika kwa mkono kurasa hizo adhimu za Qur'ani akiwa mjini Karachi.

Rassam ana timu wa wachoraji na wanakaligrafia 200 waliopata mafunzo maalumu ambayo wanashughulikia mradi huo unatazamiwa kumalizika mwaka 2026.

Kila ukurasa wa Msahafu huu  una ukubwa wa mikta 2.6 kwa  1.98 na utakapokamilika utakuwa na kurasa 550 na hiyo kuvunja rekodi ya dunia ambayo inashikiliwa na msahafu wenye kurasa za mita mbili kwa 1.52.

Katika maonyesho ya Dubai Expo 2020, Rassam anapanga kuoneysha kurasa za Sura Ar Rahman baada ya kumaliza kazi hiyo mjini Karachi katika kipindi cha siku 20 zijazo.

Hapa chini ni picha na klipu za Msahafu huo wa aina yake.

 

 

/3476003