IQNA

Maandamano ya siku ya kupambana na ubeberu wa kimataifa

Alkhamisi ya tarehe 4 Noemba 2021 imesadifiana na maadhimisho ya Aban 13 kwa kalenda ya Kiirani ambayo ni siku ya kupambana na ubeberu wa dunia humu nchini. Katika siku hii wananchi wa Iran wameshiriki katika maadamano ya kulaani ubeberu wa kimataifa unaoongozwa na Marekani. Maandamano hayo yamefanyika nje ya ubalozi wa zamani wa Marekani mjini Tehran.