Shakwe ni ndege wa familia Laridae. Watu wengi huita spishi za Sternidae shakwe pia. Spishi za Laridae zina michanganyiko ya rangi za nyeupe, nyeusi na kijivu; nyingine ni nyeupe kabisa, nyingine kijivucheusi. Ndege hawa wana domo lenye nguvu na ncha kali; domo lao ni nene kuliko lile la spishi za Sternidae. Wanaweza kuogelea na wana ngozi kati ya vidole vyao.