IQNA

Sala ya Ijumaa ya Kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Nairobi

Sala ya kwanza ya Ijumaa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka huu wa 1443 Hijria Qamaria imesalia katika Msikiti wa Jamia ulioko katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi.

Maelfu ya Waislamu walijitokeza katika sala hiyo ya Ijumaa  ambapo hakukuwa na nafasi ya kutosha katika  ukumbi wa ndani ya msikiti an uwanja wa nje msikitini na hivyo kulazimu barabara ya nje ya msikiti kufungwa ili kupatikane nafasi zaidi.