IQNA

Maandamano ya Siku ya Nakba Palestina

TEHRAN (IQNA)- Maelfu ya Wapalestina katika eneo lililozingirwa na Israel la Ukanda wa Gaza na eneo linalokaliwa kwa mabavu na Israel la Ukingo wa Magharibi Jumapili wameandamana kwa mnasaba wa Siku ya Nakba.
Tarehe 14 au 15 Mei inasadifiana na mwaka wa 74 wa kufukuzwa mamia ya maelfu ya Wapalestina kwenye ardhi zao na kesho yaani tarehe 15 Mei, utawala pandikizi wa Kizayuni uliopachikwa jina bandia la Israel, utatimiza miaka 73 tangu kupandikizwa kwake kwenye ardhi hizo za Wapalestina.